Wednesday, May 29, 2013

UPDATE: MWANA FA NA KALAPINA WAAHIRISHA SHOW ZAO ZA MWISHO WA WIKI KUTOKANA NA KIFO CHA MSANII MANGWEA...

Kutokana na habari za kufariki kwa mwanamuziki Albert Mangwair, msanii ambaye ni mmoja kati ya wana Hip Hop maarufu nchini, Mwanamuziki mwingine pia wa Hip Hop Hamis Mwin'jumah, a.k.a MwanaFA(Pichani)nametangaza kuahirisha show yake ya The Finest iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii May 31, 2013.

MwanaFA ameiambia Mdimuz Blog kwamba kuguswa kwake na taarifa hizi kumesababisha ajisikie kuomboleza kwanza, kabla maisha mengine hayajaendelea, kwa hiyo amewaomba radhi mashabiki, hasa wale waliokuwa wameshanunua tiketi, na kuwaomba wawe na subira, tarehe ya show itratangazwa tena baada ya mwili wa marehemu kuletwa na kupumzishwa,

No comments:

Post a Comment