Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni
kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa
kuwa Mangwea alikuwa pamoja na mtu aitwaye M TO THE P ambaye naye yupo
mahututi kwa sasa.
Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini
Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi
amefariki akiwa usingizini.
Akiongea na Clouds FM muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye
Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani
alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili
za kuamka.
“Sijui hata huko alitumia nini,” amesema.
Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe
yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa
wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado
hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.
Hata hivyo amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa
maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair
alikuwa amepanga kurudi leo nchini.
Awali Bongo5 ilizungumza na Bushoke anayeishi jijini Pretoria ambaye
amesema alikuwa akutane naye leo jijini Johannesburg lakini alishangaa
kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washkaji ambao ni
wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki.
“Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke.
Bushoke amesema kesho amepanga kwenda Johannesburg kujionea mwenyewe.
Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na
makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia
kwenye mitandao ya kijamii.
Kilimanjaro Lager
Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji. Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.
Ndovu Special Malt
R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many Tanzanians.
Adam Nditi
Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta #RIP #Mangwair #akaCowbama
Diva
Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?
No comments:
Post a Comment