Akiongea
na bongo movies leo asubuhi, Dr. cheni alisema kuwa baada ya kumaliza
kula chakula ambacho alipakuliwa na mmoja wa wahudumu wa sherehe hiyo
alianza kujisikia vibaya na kuishiwa nguvu na aliamua kutoka nje
kujaribu kupata hewa akidhani ladba ni joto la ukumbini ila hali
ilizidi kuwa mbaya na aliamua kutafuta maziwa akihisi labda inaweza
kuwa vidonda vya tumbo ndipo alipoanza kutapika na baadae kukumbizwa
hospitalini na ndipo alipogungulika kuwa amelishwa chakula chenye sumu.
Tulipomuuliza
labda sababu gani anahisi zinaweza kuwa zimepelekea watu hao kutaka
kumdhuru alisema kuwa, mpaka sasa hajaweza kupata jibu kamili ila
anaamini watu waliofanya hivyo wanamfahamu na wana nia mbaya sana kwake
na sio watu wema.
Dr.
Cheni alisema kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na moja ya
watu walikuwa wa kwanza kufika hospitalini baada ya yeye kupatwa na
majanga hayo ni mwigizaji Elizabeth Michael (LULU) ambaye kwa sasa yupo
karibu sana na Dr. Cheni aliyekuwa mstari wa mbele katika
kushughulikia mpaka kufanikisha suala la dhamana ya kesi iliyokuwa
inamkabili mwanadada huyo.
No comments:
Post a Comment