Rais wa Uganda Yoweri Museveni,
amesema wapenzi wa jinsia moja hawapaswi kuuawa au kudhalilishwa, huku
wabunge wa nchi hiyo wakiendelea na mjadala wa kutathmini kuhusu muswada
wenye utata wa kupinga wapenzi wa jinsia moja.
Katika matamshi yake ya kwanza hadharani, kuhusu
muswada huo, Rais Museveni amekariri kuwa suala la mapenzi ya jinsia
moja halipaswi kupewa nafasi kukita mizizi.Muswada wa awali uliowasilishwa katika bunge la Uganda, ulipendekeza adhabu ya kifo kwa wale watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja, lakini kipengele hicho kimefutwa katika muswada mpya.
Katiba ya Uganda kwa sasa inaharamisha mapenzi ya jinsia moja.
No comments:
Post a Comment