Sunday, August 11, 2013

Sheikh Ponda atibiwa hospitali Dar

Jumuiya na Taasisi za kidini ya Kiislamu nchini Tanzania imeitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini na kuwachukulia hatua watu waliompiga risasi Sheikh Ponda Issa Ponda Jumamosi mjini Morogoro Mashariki mwa nchi.
Sheikh Ponda

Sheikh huyo ambaye amekuwa katika mivutano ya mara kwa mara na serikali ya nchi hiyo alipigwa risasi baada ya kutokea vurugu kwenye mkutano wa mawaidha ya baraza la sikukuu ya idd el fitr.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Alhajj Mussa Kundecha, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam Jumapili jioni kuwa endapo serikali haitachukua hatua itakayowaridhisha Waislamu, wataamua kufikiria upya mustakabali wao na serikali ya Tanzania.
Sheikh Ponda amelazwa katika hospitali ya taifa, Muhimbili, mjini Dar es Salaam kwa matibabu huku akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu.

No comments:

Post a Comment