Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta
umefungwa baada ya moto mkubwa kutokea katika uwanja huo mjini Nairobi.
Kwa sasa moto huo umeweza kudhibitiwa
Rais
Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja huo na anatarajiwa kuhutubia
waandishi wa habari baadaye. Hadi kufikia sasa hakuna ripoti zozote za
majeruhi .Mamlaka ya uwanja huo imesema kuwa tayari watu waliokuwa katika eneo hilo wameondolewa.
Imesema kuwa baadhi ya operesheni za uwanja huo zimekatizwa huku ndege zinazoingia katika uwanja huo zikielekezwa kutua katika viwanja vingine ndege kama vile Entebe, Dar es Salam ,Kigali, Mombasa na kwingineko nchini Kenya.
Baadhi ya safari za ndege kutoka uwanja huo pia zimeahirishwa.
Mwishoni mwa wiki jana baadhi ya wenye maduka ya Duty Free katika uwanja huo walifurushwa baada ya serikali kusema kuwa leseni za wenye maduka zilikuwa zimepitwa na muda.
Hata hivyo chanzo cha moto bado hakijabainika.
No comments:
Post a Comment