Tukio la bomu la Arusha limewasitua wengi kufuatia vifo vya wananchi wanne wasio na hatia....
Nasema hawana hatia kwa sababu siku
ya tukio wananchi hao walikuwa katika mkutano wa hadhara wa
chama chao ( CHADEMA ) sawa na ambavyo wangeweza kuwa katika
mkutano mwingine wowote wa kisiasa....
Pamoja na majonzi waliyonayo
wananchi, wanasiasa wetu wanaonekana kutoguswa kabisa na vifo
hivyo ambavyo kwa mtazamo wangu nathubutu kusema kuwa chanzo
cha yote ni wao .....
Jana kupitia account yake ya
twitter, mbunge Serukamba alidai kuwa tukio la Arusha halimpi
fundisho lolote zaidi ya fundisho moja tu kwamba TANZANIA KUNA
WANARIADHA WAZURI.....
Tunapata fundisho gani hapa???...
Ndugu zetu wamekuwa wakipoteza maisha kila mara kupitia mikutano
ya wanasiasa wetu....
Cha kushangaza ni kwamba, wanasiasa haohao wamekuwa wakitucheka na kutudhihaki...!!!
Kauli hii ni fundisho tosha.
Tukio la Arusha limesibitisha pamoja mambo mengine kuna vipaji vilivyojificha kwa watu wengi hasa kwenye mchezo riadha!
— peter serukamba (@serukamba) June 19, 2013
Najaribu kuihusisha kauli ya mbuge huyu na tusi la nguoni alilowahi kulitoa bungeni la "COME ON FU**K U"...ili nimjue alivyo
Matukio haya yanatosha kumpima Serukamba na kumjua jinsi alivyo...!!!
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/06/tukio-la-arusha-limenifanya-niamini.html#ixzz2WlmWaCvq
No comments:
Post a Comment