Awali ya yote ningependa kutanguliza shukrani kwa mwenyezi Mungu
aliyeniwezesha mimi na team yangu nzima ya wasafi kusafiri na kufika
salama visiwani Comoro,lakin pia siwezi acha kuwashukuru mashabiki wangu
wa kweli kwa dua wanazoendelea kuniombea..tulifika Comoro mapema jioni
na kupokelewa na umati wa watu waliokuwa an hamu ya kumwona mtoto wa
kitanzania nikitua nchini mwao hizi ni baadhi ya picha za matukio jinsi
wana Comoro walivyonipokea
Ukweli ni mara yangu ya kwanza kufika Comoro na nilifurahishwa na ukarimu wa watu hawa na jinsi
walivyonipokea vyema kweli Africa yote ni ndugu wa baba mmoja
Baadaya kutoka Airport nilifanyiwa mahojiano na kituo cha televisheni cha nchini Comoro
No comments:
Post a Comment