MCHUNGAJI mmoja wa kanisa la Church elders of Faith Ministries Nchini
Zimbabwe amejikuta akivuliwa wadhifa wake huo mtakatifu mara baada ya
kugundulika kuwapa mimba wake za watu sita katika nyakati tofauti
tofauti katikakipindi cha mwaka mmoja...!!
"Kitu
alichokifanya mchunagaji huyu ni kibaya sana na mtu kama yeye hatakiwi
kabisa kuwa sehemu ya kanisa kwa sasa, kwasababu kile alichokifanya ni
kinyume kabisa na maadili ya UKRISTO.Kuna baadhi ya watu wenye hasira kali walitaka kumpiga lakini bahati nzuri wazee wa kanisa waliwazuia "..alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliyeonekana kuchukizwa na kitendo cha mchungaji huyo
Wahubiri katika kanisa hilo
walivujisha kuwa katika kanisa hilo kuna kiongozi mkubwa ambaye ana
tabia ya kulala na wake za watu na alipokuja kuulizwa kuhusiana na hilo
mchungaji huyo alikuwa na haya ya kusema:
"Najisikia
vibaya sana na ningependa kuomba msamaha kwa hili nililolifanya na kama
nikipewa nafasi nyingine naahidi kutorudia tena. Vile vile nakubaliana
na maamuzi ya wazee wa kanisa kuamua kunivua wadhifa wangu mtukufu"... alimalizia mchungaji huyo ambaye alionekana kuwa na majonzi ya kutosha.
No comments:
Post a Comment