Sunday, June 30, 2013

"BODA BODA NI SERA YA CCM KUSAIDIA VIJANA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AJIRA "..LOWASA

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.

Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.

Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.

“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni cha kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.

Lowassa alisema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba wasipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.

“Ndiyo maana CCM katika ilani yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.

Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.

Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 10

No comments:

Post a Comment