HAYA ni madai mazito! Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Kijito cha
Utakaso au Healing Centre International lililopo Kimara-Mwisho, Dar,
Thomas Mariki anadaiwa kuvuliwa kofia ya uchungaji baada ya kutuhumiwa
kuzaa na ‘hausigeli’ wake, Sessy Mwambashi.
Akizungumza nasi Jumamosi kwa masikitiko, mke wa ndoa wa Mariki,
Joyce Thomas Mariki alidai kuwa yeye na mchungaji huyo walioana mwaka
2004 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa
Lungai Mwika, Moshi.
Alisema walijaliwa kupata watoto watatu lakini mmoja hakuwa bahati.
MATESO YAANZA
Mwanamke
huyo alidai amani katika ndoa yake ilipotea baada ya kujifungua mtoto
wa pili (marehemu), mumewe alianza kumtuhumu kuwa alitoka nje ya ndoa na
huyo mtoto hakuwa wake.
Aliendelea kudai kuwa, mtoto alipofikisha
mwaka mmoja na miezi nane, walishauriana watafute hausigeli ili mama
huyo afanye biashara ya kuwaongezea kipato.
Mama mchungaji alisema alimpata Sessy akiwa na miaka 15, mkazi wa Mbozi, Mkoa wa Mbeya.
Alisema
yeye alianza biashara ya genge maeneo ya Kimara-Mwisho ambapo alikuwa
akiwahi sokoni saa 11:00 alfajiri na kumwacha msichana huyo akiendelea
na kazi za nyumbani.
VISA VYAANZA
Mama mchungaji aliendelea
kudai: Baada ya miezi michache, mchungaji alibadilika tabia, alikuwa
mkali, wakati mwingine alinifuata sokoni na kunipiga akinishutumu nina
uhusiano na wanaume ndiyo maana nachelewa kurudi nyumbani.
MUMEWE AMFICHULIA SIRI
Akadai:
“Siku moja mchungaji alinifichulia siri kuwa hausigeli wetu ni mjamzito
na mimba ilikuwa yake hivyo akataka iwe siri kati yetu watatu.”
Mama
Mariki alisema alikubaliana na mumewe ambapo alivumilia kwa kipindi
kirefu lakini uzalendo ulimshinda baada ya msichana huyo kuwa na tabia
ya kuwatesa watoto huku akisema aachwe kwani ni mjamzito.
MKE NAYE AFICHUA SIRI
Alisema
kuwa baada ya kuona mumewe anamjali zaidi hausigeli kuliko yeye na
watoto aliamua kwenda kutoa siri kwa wasimamizi wa ndoa, wakaitwa na
kusuluhishwa ambapo waliamua kuwa msichana huyo arudishwe nyumbani kwao
Mbeya jambo ambalo mtumishi huyo wa Mungu alilitekeleza, yeye mwenyewe
alimrudisha msichana huyo kwao.
NDOA YATIBUKA
Mwanamke huyo
alidai mumewe huyo aliporudi Dar, alianza visa akisema kuwa hausigeli
alikuwa akimpa ‘mambo’ kuliko yeye ambaye amezeeka huku vitisho na
vipigo vikiongezeka maradufu!
“Wasimamizi wa ndoa walituita kwa mara
nyingine wakatusuluhisha lakini tulipofika nyumbani, mateso yakawa
palepale ndipo wasimamizi waliponiambia nirudi kwa wazazi wangu kwani ni
aibu kubwa kwa mtumishi wa Mungu kufanya vile,” alisema na kuongeza:
“Kweli
nilirudi kwetu Moshi, wazazi wangu walimpigia simu mume wangu kuhusu
matatizo yetu, lakini aliwajibu hanitaki na ataniletea talaka nyumbani.”
Alisema miezi mitatu baadaye, wasimamizi wa ndoa walimtaka arudi Dar kwa ajili ya kujua hatima ya ndoa yake.
Aliambatana
na kaka yake hadi nyumbani kwa mumewe, cha ajabu walimkuta hausigeli
akiwa na mtoto mchanga. Aliwazuia kuingia ndani akidai hawakuwa na
mamlaka hayo.
Alisema kaka yake alimtaka hausigeli ampigie simu
mchungaji amwambie shemeji yake anamhitaji, alifanya hivyo na mchungaji
alifika lakini alipowaona alitoka nduki.
WAZEE WA KANISA WAINGILIA KATI
Aliendelea
kudai kuwa ulifika wakati wazee wa kanisa waliingilia kati, wakamuweka
mchungaji kikao na kumuuliza kulikoni hawamuoni mke nyumbani badala
yake msichana wa kazi tena akiwa na kichanga.
“Cha kushangaza
mchungaji alipandwa na hasira, akawafanyia fujo wazee hao, alimpiga na
kiti mzee mmoja ambaye alikuwa msaidizi wake anayeitwa Kisaka na
kumjeruhi,” alisema mama mchungaji.
Alisema sakata la kujeruhiwa kwa
Kisaka liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Mbezi Kwayusuf na
kufunguliwa jalada namba KMR/RB/2125/2013- SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
AVULIWA UCHUNGAJI
Alisema katika kikao hicho, wazee hao walifikia uamuzi wa kumvua rasmi uchungaji kwa kumwandikia barua na kumkabidhi.
Mchungaji
aliipokea barua hiyo lakini hadi sasa anaendelea na huduma kwani wapo
waumini wachache walio upande wake huku wengine wakidaiwa kulikimbia
kanisa hilo.
BOFYA HAPA UMSIKIE MCHUNGAJI
Baada ya kuzinyaka
habari hizo, Juni 18, mwaka huu, mapaparazi wetu walimtafuta Mchungaji
Mariki na kufanikiwa kumkuta nyumbani kwake Kimara-Mwisho ambapo alikuwa
na haya ya kusema:
“Siwezi kuzungumzia lolote kuhusu habari
alizosema mke wangu kwa sababu suala hili lipo kwenye Baraza la
Usuluhishi wa Ndoa na lipo kwa maandishi, naweza kuwaambia kuwa kuna
watu wanataka kunipindua, wanapanga hila na njama ili walichukue kanisa
na ndiyo wanamtumia mke wangu lakini hawawezi, wameshindwa.
“Kuhusu
kuzaa na hausigeli wangu ni kweli na mtoto ana miezi saba sasa, lakini
hizo shutuma kwamba alikuwa na miaka 15 siyo kweli, alikuwa na miaka 17
na sasa ana miaka hiyohiyo.”
HAUSIGELI VIPI?
Risasi Jumamosi
lilizungumza pia na hausigeli ambaye anaishi na mchungaji huyo kwa sasa
kama mke ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Anayesema nilikuwa na
miaka 15 ana ushahidi? Wanaoweza kujua umri wangu ni wazazi wangu na
ukweli ni kwamba mwezi wa kumi mwaka huu natimiza miaka kumi na nane.
“Kuhusu
kwamba nilikuja kufanya nini Dar, nilikuja kwa mume wangu mwenye
ushahidi kuwa nilimfukukuza mke wake alipokuja nyumbani aniletee.”
Hata hivyo, Risasi Jumamosi linaendelea kufuatilia sakata hili ili kukujuza nini hatima yake.
SOURCE: RISASI JUMAMOSI
No comments:
Post a Comment