Mahakama
ya Rufaa imemrejeshea ubunge aliyekuwa mbunge wa Sumbawanga Mjini,
Aeshi Hilaly (CCM)baada ya kung'amua mapungufu ya kisheria katika maamuzi ya
Mahakama Kuu iliyokuwa imemnyang'anywa kiti hicho.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali aliiomba Mahakama ya Rufaa kumrudishia ubunge Hillaly
akisema hakuna uthibitisho kwamba alihusika kutoa rushwa wala kufanya
vurugu katika kampeni za uchaguzi za mpinzani wake.
Akimwakilisha
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili wa Serikali Mkuu, Michael Luena
akishirikiana na Wakili wa Serikali, Karim Rashid waliomba mahakama
itengue hukumu iliyotolewa na Jaji Bethuel Mmila wa Mahakama Kuu, Kanda
ya Sumbawanga ambayo ilimuondoa madarakani Aeshi.
Aprili 30 mwaka
jana, Jaji Mmila alitengua matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Aeshi
kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo
hilo kwa tiketi ya CHADEMA, Norbet Yamsebo.
“Waheshimiwa majaji
tuna hoja 10 za kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Sumbawanga...
katika hoja hizo tutaangalia mambo matatu ambayo yanahusu dhamana ya
kufungulia kesi ya uchaguzi, kuwapo vurugu wakati wa kampeni na kuwapo
rushwa,” alidai Luena.
Akiwasilisha hoja ya kuwekwa kwa dhamana
ya kufungulia kesi kama sheria inavyoelekeza, Wakili Karim alidai kuwa
Yamsebo hakuweka dhamana hiyo hivyo anaiomba Mahakama ya Rufani itengue
aumuzi uliotolewa wa Mahakama Kuu katika kesi ya uchaguzi.
Kuhusu
hoja ya vurugu, Luena alidai kulikuwa na mkanganyiko mkubwa katika
ushahidi wa mashahidi wa mlalamikaji (Yamsebo), ambako wengine walidai
mkutano wa kampeni ulifanyika lakini wengine walidai haukufanyika kwa
sababu ya vurugu.
No comments:
Post a Comment