Tuesday, September 24, 2013

Mashambulizi ya kigaidi Afrika Mashariki



Mlipuko uliosababishwa na Al Shabaab Somalia

Haya ni miongoni mwa mashambulizi makubwa ya kigaidi ambayo yamewahi kutekelezwa katika kanda ya Afrika Mashariki.
Septemba. 21, 2013: Magaidi walitumia maguruneti na bunduki kushambulia jengo la kifahari la Westgate mjini Nairobi, Kenya lenye maduka na mikahawa themanini na kuwaua watu zaidi ya sitini huku zaidi ya 175 wakijeruhiwa.Kundi la kigaidi la Al-Shabab lilikiri kufanya shambulizi hilo.
___

Oktoba 2011-Machi 2013: Al Shabaab na wapiganaji wake walifanya mashambilizi kadhaa nchini Kenya na kuwaua zaidi ya watu sitini wakilipiza kisasi kile walichosema ni hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini huo kupigana dhidi yao. Serikali ya Kenya ilituma vikosi vyake nchini Somalia baada ya al-Shabab kufanya mashambulizi kadhaa katika maeneo ya mipakani pamoja na kuwateka nyara watalii wa kigeni.
___
Mnamo mwezi Julai tarehe 11,mwaka 2010: Wanamgambo wa Al Shabaab walilipua misururu ya mabomu katika mji mkuu wa Uganda Kampala, katika mkahawa ambako mashabiki wa soka walikuwa wanatizama fainali ya michuano ya kombe la dunia, kwenye skrini kubwa. Takriban watu 76 waliuawa. Kundi la Al-Shabab lilisema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Uganda kujihusisha na vita dhidi ya kundi hilo Somalia.
___

Tarehe 28 mwezi Novemba, mwaka 2002: Kundi hilo la kigaidi lilishambulia hoteli ya kifahari iliyokuwa inamilikiwa na waisraeli, katika eneo la Kikambala karibu na mji wa Mombasa na kuwaua watu 13. Dakika chache kabla ya shambulii hilo, magaidi hao waliifyatulia makombora ndege ya kiisiralei iliyokuwa inaruka katika uwanja wa kimataifa wa Mombasa, lakini waliikosa.
___

Mnamo tarehe saba Agosti, 7 mwaka 1998: Kundi lengine la kigaidi la Al-Qaida ilishambulia balozi za Marekani mjini Nairobi na Dar es Salam. Mashambulizi hayo yaliwaua watu 224 , wengi wakiwa wakenya . Raia 123 wa Marekani pia waliuawa. Wengine wengi pia walifuawa nchini Tanzaia.

No comments:

Post a Comment