MGANGA wa jadi, George Tereva (55) mkazi wa Kijiji cha
Lungemba wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa ameuawa kikatili
baada ya watu wasiojulikana kwenda nyumbani
kwake na kupiga risasi tatu katika maeneo
ya tumboni, kichwani na kwenye paji lake la uso.Pia watuhumiwa
hao walimcharanga mganga huyo kwa panga kichwani na
kutoweka bila kuchukua mali zozote za
marehemu huyo
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi Mkoa wa Iringa, Dkt.
Galus Msekwa akizungumzia tukio la kuuawa kwa mganga
mwenzao, George Tevere ambaye alikuwa
anawatibu wagonjwa kimeisikitisha jumuiya yao mkoani humo.
"Watu walikwenda kwa mganga huyo kuomba gari kwa malengo ya
kutaka wasafirishiwe mgonjwa wao hadi anapoishi mganga huyo,
lakini alipotoka ndani ya nyumba ili awasikilize ndipo walipoanza
kumshambulia kwa kumpiga risasi tumboni;"Kichwani
na baadaye kuanza kumcharanga kwa mapanga katika maeneo ya mwili wake
hasa kichwani hadi kusababisha kifo chake, suala hili limetushtua
sana," alisema Dkt. Msekwa.
No comments:
Post a Comment