MBUNGE
wa Masasi mkoani Mtwara, Mariam Kasembe (CCM) jana alimwaga machozi
mbele ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alipotembelea kuona
uharibifu wa mali na nyumba za mbunge huyo zilizochomwa na wananchi
mapema mwaka huu. Waziri Maghembe ambaye yupo mkoani hapa kwa ziara ya
siku tano kukagua miradi ya maji, alifika nyumbani kwa mbunge jana
asubuhi, kabla ya kwenda Wilaya ya Nanyumbu.
Mariamu alianza kumwaga chozi baada ya Waziri Maghembe na msafara wake, kufika mbele ya nyumba yake iliyoteketezwa kwa moto na wakati wa vurugu zilizotokea mwaka huu.
“Mheshimiwa waziri kama unavyoona, hii ndiyo hasara niliyopata, nyumba yote imekwisha naisha maisha kama mkimbizi.
“Mali zangu zimeharibika unaona ile trekta pale haina kazi, gari langu limebaki vyuma chakavu… nina wakati mgumu kurudi katika hali ya kawaida,”alisema Mariamu huku akilia.
Alisema mpaka sasa baadhi ya wanafamilia wake wanaishi kwenye kontena ambalo liko ndani ya uzio wa nyumba yake ambayo imebaki gofu.
“Ninyi waandishi mbona mnapita hili kontena, hii ni nyumba yangu jamani ipigeni picha…namuachia Mungu,”alisema Mariamu ambaye alifuatana na mume wake.
Naye Waziri Maghembe aliwaomba viongozi wa Halmashauri ya Masasi na Mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi kutafuta kila aina ya njia kumsaidia mbunge huyo.

No comments:
Post a Comment