Wednesday, August 7, 2013

FLORA MVUNGI: MTOTO WANGU ATAITWA TANZANITE.

 MSANII wa filamu na muziki Bongo, Flora Mvungi amekubaliana na uamuzi wa mumewe ambaye ni msanii wa muziki na filamu, Hamisi Ramadhani Baba ‘H. Baba’ kwamba  mtoto wao mtarajiwa atapewa jina la Tanzanite.
Flora alisema mumewe alichagua jina hilo kwa sababu mtoto wao huyo anatarajiwa kufahamika kimataifa kutokana na umaarufu atakaokuwa nao na ikizingatiwa kuwa madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania pekee.
“Kama nikijifungua salama awe mtoto wa kiume au wa kike ataitwa jina hilo na atakuwa tofauti sana na msanii wa muziki anayejiita Tanzanite kwa kuwa yule hilo siyo jina lake halisi bali ni a.k.a tu,” alisema Flora.
Flora na H: Baba walifunga ndoa hivi karibuni na wakati wowote wanatarajiwa kupata tunda lao la kwanza kwani Flora ni mjamzito.

No comments:

Post a Comment