Tuesday, July 23, 2013

WATU 40 WANUSULIKA KUFA AJALI YA BASI LA MOHAMED TRANS

Abiria zaidi ya 40 waliokuwa wakitoka Dodoma mjini kuelekea jijini Mwanza leo wamenusurika kufa baada ya basi la kampuni ya Mohammed Trans lenye namba za usaji T 210 APG, kupata ajali kwenye mzunguko (round about) ya peoples klabu mjini Singida.

Baadhi ya abiria wamepata majeraha madogo madogo.
Imedaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.Picha na Nathaniel Limu Wa dodoma.

No comments:

Post a Comment