Wednesday, July 10, 2013

HII NIKALI YA MWAKA JAMAA AFANYA VURUGU KWANDUGU ZAKE , KISHA AJINUNULIA JENEZA


KIJANA Lusajo Kabuje mkazi wa kitongoji cha Isanga Kijiji cha Iwindi, Wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa, ameonekana na jamii kuwa ni mtu wa ajabu na amekamatwa na polisi kabla ya kutekeleza mpango wake wa kufanya mauaji ya kutisha kwa ndugu zake.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi  saa 11.24 jioni eneo la klabu cha pombe, Isanga Julai 2, mwaka huu huku akiwa na visu viwili ambavyo alikusudia kufanyia unyama huo huku akiwajeruhi polisi waliofika kumkamata kabla hajatekeleza nia yake hiyo ovu.
Mwandishi wa habari hizi baada ya kupata taarifa juu ya nia ya mtuhumiwa kuua nduguze kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Iwindi, Anyelwisye Mwaisela, aliyemuomba mwandishi kutoa taarifa polisi, aliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, ACP Diwani Athumani ambaye alituma askari na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.


Kabla Lusajo hajakamatwa, alifanya vurumai kubwa ambapo alimjeruhi askari mmoja mkononi, hata hivyo walifanikiwa kumdhibiti na akafungwa pingu.
Baada ya kukamatwa tulifika nyumbani kwake na kukuta jeneza, msalaba, katoni ya chumvi na mafuta ya kupikia ambavyo vyote tuliambiwa na mkewe kuwa aliviandaa kwa ajili ya mazishi yake, hakika huyu ni mtu wa ajabu,” alisema askari mmoja aliyehusika kumkamata.
Baba mzazi wa Lusajo, Emmanuel Kabuje alimwambia mwandishi wetu kuwa kijana wake hajawahi kuwa na matatizo ya akili lakini Juni 28, mwaka huu alimtishia kumuua kwa kumkatakata vipande kwa shoka na akatoa taarifa polisi Kituo cha Mbalizi.


 Oliver Mwaluanda (pichani) ambaye ni mke wa mtuhumiwa alisema: “Alipania kuniua mimi, baba yake, dada yake kutokana na wivu, ndugu zake walikuwa wakinitetea, alinunua jeneza lake kwani alisema akituua naye atajiua.

No comments:

Post a Comment