Sunday, June 16, 2013

Wazinzi mwanza wapatanishwa kwa kufanya sherehe kubwa Mwanza

Katika hali ya kushangaza hapa mwanza ktk eneo la nyakato ktk Bar ya S&D jana kulifanyika sherehe kubwa ambayo iliambatana na uchinjaji wa ng'ombe wawili na vinywaji mbalimbali ikiwemo kreti 50 za bia ili kuwapatanisha wafanyabiashara wawili ndg. Riziki na ndg. Maduhu ambao walipigana mwezi uliopita na kujeruhiana vibaya ktk sehemu mbali mbali za mwili na hata kufikisha ktk vyombo vya sheria hali iliyotokana na kugombania mwanamke anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu. Je ni sahihi kweli kufanya sherehe kwa jambo la kipuuzi kama hili na kupoteza fedha nyingi kiasi hiki kwa watu wasio wadhirifu ktk ndoa zao ?.

No comments:

Post a Comment