KATIKA kuonesha kuwa bado uaminifu kwa wapenzi ni tatizo, juzikati
lilitokea fumanizi la aina yake baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika
kwa jina la Flaviana kumnasa mwanaume aliyedaiwa ni mumewe, aitwaye Aron
akifanya mapenzi na mwanamke mwingine.
Tukio hilo lililowashangaza
wengi lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika gesti moja iliyopo
Sinza jijini Dar. Awali Flaviana na bwana wake huyo walichukua chumba
baada ya kushindwa kurudi nyumbani kutokana na kuzidiwa na kilevi.
Ilikuwaje fumanizi likatokea?
Ilielezwa
kuwa wakati wawili hao wakiingia kwenye chumba cha gesti hiyo, Flaviana
alikuwa bwii hivyo ‘kuzima’ kwenye kochi na kushindwa kufanya chochote.
“Wakati
Aron akiwa chumbani pale, alifika shosti wa Flaviana aitwaye Dina na
kwa kuwa Flaviana alikuwa hajitambui, wawili hao walianza kupeana
malavidavi.
“Flaviana akiwa amelala alikuwa kama vile anasikia watu
wakishughulika lakini alishindwa kufanya chochote kutokana na kuzidiwa
na pombe.
“Wale wakaendelea kubanjuka. Ilipofika saa 12 asubuhi
Flaviana akapata nguvu na kuamka kwenda kujisaidia, aliporudi akabaini
shosti wake amemsaliti na ndipo alipoanzisha timbwili,” alidai mtoa
habari wetu.
Flaviana apigia simu mapaparazi
Wakati timbwili
hilo likiendelea chumbani hapo, Flaviana alipata mwanya wa kuwapigia
simu mapaparazi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshuhudia Dina
akiwa ndani ya Bajaj huku akivaa nguo kabla ya kumuamuru dereva kuondoka
kwa spidi.
Naye mwanaume ambaye alikuwa ndani ya chumba cha gesti
hiyo, aliposikia waandishi wamefika, alitokea mlango wa nyuma akiwa
amevaa ‘boksa’ na tisheti, akaacha suruali yake chumbani hapo.
Akizungumza
na Risasi Jumamosi huku akiwaonesha mapaparazi kitanda kilichokuwa
vululuvululu, kilichotumika katika usaliti huo pamoja kondom, Flaviana
alisema: “Nimeumia sana, yaani nimesalitiwa nikiwa humuhumu chumbani,
Aron kanidhalilisha sana na huyo Dina naye kumbe siyo mtu, nitahakikisha
namsaka nimshikishe adabu.”
No comments:
Post a Comment