Imethibitika kwamba technology ya mawasiliano hivi sasa imekua kwa kasi
ya ajabu sana, kiasi chakufikia kuwa kumbe siyo lazima tutegemee camera
za waandishi wa habari kuchukua matukio.
Ni kwamba chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwenye mkutano wake
wa mwisho licha ya kutumia SATELLITE kurekodi mikutano yake, imethibitika
kuwa chama hicho kilitumia mtambo maalum wa mawasiliano kurekodi mkutano
wake wa mwisho katika uwanja wa soweto Arusha. Mtambo huo ambao
unauwezo wa kurekodi matukio kwa masaa 72 mfululizo bila kuhitaji chaji,
ulifungwa sehemu maalum ili kuweza kunasa matukio yaliyokuwa
yanaendelea kwenye mkutano.
Mtambo huo ulisaidia kunasa tukio la mlipuko wa bomu na matumizi ya
risasi kwenye mkutano kuwapiga raia, ambapo ulionyesha askari polisi
aliyesimama pembeni ya nguzo ya umeme karibu na mfereji ulio mkabala na
round about iliyo karibu na soweto garden akiwapiga risasi watu
waliokuwa wanamkimbiza mtu aliyevaa suruali ya jeans aliyekimbia
nakuingia kwenye gari ya polisi na kuondoka kwa kasi kwenye eneo la
tukio. Mtambo pia uliweza kuonyesha gari ya blue landcruiser iliyoweza
kui escort gari ambayo amepanda tule mtu aliyekuwa anakimbizwa.
Ule mtambo ambao una uwezo wa kurekodi matukio kwa around 360 degree
angle uliweza kuonyesha tukio la watu wanaosadikiwa kuwa maaskari kufika
kwenye eneo la tukio hasa kwenye gari la matangazo la chadema majira ya
usiku, na kuweza kuzurura pale bila kuonyesha kwa kina walichokuwa
wanakifanya pale.
No comments:
Post a Comment