Mwimbaji kutoka Tanzania House of Talent (THT) Barnabas Elias maarufu
kama Barnaba amefiwa na mama yake mzazi alfajiri ya leo jijini Dar es
salaam.
Taarifa zilizothibitishwa na rafiki wa karibu na msanii mwenzake
Amini , zinasema mama yake Barnaba amefariki nyumbani kwake alfajiri ya
leo Jumamosi (June 22) kutokana na presha.
Tunawaombea ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na familia ya Barnaba
ambao wako katika kipindi hiki kigumu na Mungu alizae mahala pema roho
ya marehemu, Amen.
No comments:
Post a Comment