WATU wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokuwa wamevaa kikekike
wameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuwakurupusha wakivunja
duka usiku.
Mauaji hayo yalitokea eneo la Nyegezi Kijiweni, Kata ya
Mkolani, wilayani Nyamagana jijini Mwanza, majira ya usiku, Mei 29,
mwaka huu wakiwa katika harakati za kuvunja maduka matatu yaliyopo eneo
hilo.
Watu hao ambao ni wanaume wanadaiwa siku ya tukio wakiwa na
silaha ya moto (bunduki) walivunja nyumba tatu na duka moja katika eneo
hilo kwa kutumia vifaa mbalimbali vya jadi.
Imedaiwa kuwa wakati
majambazi hayo manne yakifanya uhalifu huo, mawili yalivaa makoti meusi
marefu na yaliyobaki yalijitanda ushungi na kujifunga kanga na kujipaka
wanja usoni ili yasitambuliwe.
Chanzo hicho kilieleza kuwa majambazi
wawili waliokuwa na silaha ya moto, baada ya kukurupushwa walikimbia na
kutokomea kusikojulikana.
Wananchi kuona hivyo waliwadhibiti waliovaa mavazi ya kike na kuwashambulia kwa kuwakatakata kwa mapanga hadi kuwaua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna (DCP) Ernest Mangu
(picha ndogo), alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
uchunguzi unaendelea.
No comments:
Post a Comment