Marehemu Magwair mwigizaji na mwanamuziki
UNAPOONGELEA moja kati ya filamu bora ni filamu ya Copy iliyotwaha tuzo
tano, leo tunaongelea filamu hiyo ikiwa ni katika kumuenzi mwanamuziki
na mwigizaji wa filamu Bongo Albert Mangweha ‘Ngwair’ aliyefariki nchini
Afrika ya kusini, na kuzikwa siku ya alhamisi mkoani Morogoro katika
makaburi ya Kihonda.
Ngwair enzi mwigizaji aliyeshiriki filamu ya Copy.
Msanii huyu pamoja na kuvuma sana katika muziki wa kizazi kipya
lakini pia alikuwa mahiri katika uigizaji wa filamu lakini si watu wengi
wanalijua hilo Mangweha alishiriki katika filamu ya Copy iliyoshinda
tuzo tano zilizoandaliwa na kampuni ya One Game Promotion ya Jijini Dar
es Salaam.Baada ya kufanya vizuri katika filamu ya Copy niliwahi kuongea na mpiga wa filamu hiyo kuhusu marehemu Mangweha kutokana na umahiri alionyesha katika filamu ya Copy, kwani hakupenda kushiriki katika zingine mara kwa mara pamoja na watayarishaji wa filamu hiyo kummwagia sifa kuwa ni mwigizaji mwenye uwezo mkubwa tofauti na msanii yoyote unayemjua, naye alisema.
.
Kelvin mtunzi na muongozaji wa filamu ya Copy.
“Najua kama nina uwezo wa kuigiza lakini najali sana taaluma na
kuheshimu kazi ya mtu mwingine sipendi kushiriki kila filamu kutokana na
hadithi husika, lazima nisome Script na kuielewa kama ni nzuri hilo
ndio lilotokea katika filamu ya Copy niliipenda story yake ilikuwa nzuri
na ya kuvutia,”alimnukuu Rashid Mrutu.Mangweha atakumbuka sana katika tasnia ya filamu kwani inaaminika kuwa filamu ya Copy aliyoigiza akiwa kama mwigizaji msaidizi akiwa na Kelvin ambaye ni kinara wa filamu hiyo mchango wake ulisaidia filamu hiyo kushinda tuzo tano na kuwa filamu bora kwa 2007/ 2008 kama mshindi wa jumla baada ya kushinda tuzo nyingi.
.
Ngwair katika pozi la picha.
Rashid Mrutu mpiga picha mahiri aliyerekodi filamu ya Copy
“Mangweha ni zaidi ya msanii wa filamu, mara nyingi unapomshirikisha
katika filamu msanii ambaye hajawahi kuigiza na kumpa nafasi kubwa kazi
huwa ngumu na kuchosha lakini, Mangweha hatukuwa na muda wa kurudi
scene, kwani alishika script vema na hakukosea wala kuongeza maneno
ambayo hayakuwepo katika script,”anasema mtunzi wa filamu hiyo ya Copy
Kelvin.Rashid Mrutu ambaye alikuwa mhariri na mpiga picha wa filamu hiyo amesema kuwa Mangweha alivaa uhusika katika filamu hiyo na kumfanya mshiriki mwenzie ambaye ni Kelvin kuigiza kwa hisia zaidi na kuifanya kazi hiyo kuwa bora na kuibuka mshindi hizo tuzo tano.
.
Kelvin akiwa na mkewe nikita wakipokea moja ya tuzo za Vinara.
“Albert ni mwigizaji wa aina yake katika waigizaji ambao wanamuziki
niliofanya nao kazi za filamu hakuna kama yeye, naamini kabisa kama
angeamua kuingia moja kwa moja katika filamu basi angewafunika wasanii
nyota, kwani anatii muongozaji na kufuata script huku akivaa
uhusika,”anasema Mrutu.Mangweha katika filamu ya Copy aliigiza kama rafiki wa Kelvin ambaye alikuwa mchumba wa Janeth (Elizabeth Chijumba), akipata upinzani kutoka kwa mwigizaji Richie Richie ambaye kutokana na fedha anamtaka Janeth bila mafanikio na kujikuta akitumia nguvu za giza ili ampate Janeth anayempenda Kelvin rafiki wa Mangweha.
Katika filamu hiyo JB ameigiza kama baba yake mzazi wa Janeth ambaye pia anamtaka Ritchie na si Kelvin kwa sababu anahisi kuwa hana fedha na mwanaye asingependa aolewa na maskini mtafaruku unaanzia hapo na kuingia nguvu za giza.
Pamoja na kukutana na nyota wa filamu Bongo kama vile JB, Mzee Olotu, Mama Njaidi, Kelvin, Single Mtambalike, Aunt Fifi, Muhogo Mchungu, lakini ngweiar alionyesha uwezo mkubwa na kuwa kivutio kwa wasanii hao ambao walitamani kumshirikisha katika filamu zao lakini kutokana na msimamo wake ilikuwa ngumu.
Katika filamu ya Copy msanii mwingine kutoka kundi la Chemba Squad ambaye naye alishiriki katika filamu hiyo kama mlinzi wa kimasai alikuwa ni Dack Master, ambaye naye alionyesha umahiri katika nafasi hiyo hata baadhi ya watu kuwashawishi kama muziki wakiona unawasumbua basi waigie katika uandaaji wa filamu na kuwashirikisha wanachemba wote.
Jambo lilojitokeza ni toka siku iliyotokea kifo cha msanii huyo tarehe 28 mwezi May mwaka huu, nakala ya filamu hiyo imetafutwa katika maduka maarufu ya uuzaji wa filamu haipatikani, awali ilikuwa ikisambazwa na kampuni ya Kapico baadae iliuzwa na kampuni ya Steps ambao wamesimama kuizalisha.
Filamu ya Copy ilinyakua tuzo ya kuwa filamu bora ya mwaka 2007-2008, katika shindano la tuzo za vinara wa filamu Tanzania Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
.
Marehemu Ngwair enzi za uhai wake.
Filamu hiyo ilinyakua tuzo tano kupitia kwa Khalfan Ahmed ‘Kelvin’
aliyenyakua tuzo mbili za Mtunzi bora na Muongozaji Bora, Rashid Mrutu
aliyenyakuwa tuzo mbili za mpiga picha Bora na Mhariri Bora na
Elizaberth Chijumba ambeye alinyakuwa tuzo ya kuwa Mwigizaji bora wa
Kike.Tasnia ya filamu na muziki imepoteza msanii muhimu wakati filamu na muziki zikielekea katika urasimishaji na kuwa sekta rasmi, pengine inawezekana wasanii wakajikomboa baada ya kuibiwa kazi zao na maharamia na kujikuta wakiingia katika msongo wa mawazo, Bwana ametoa, Bwana katwaha jina lake lihimidiwe, Mungu ilaze roho ya marehemu Albert Mangweha mahali pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment