CHUO Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM) kimekanusha madai kwamba wanafunzi wake ni makahaba wanaofanya vitendo vya ngono na mbwa.
Kwenye
barua ya kukana dai hilo iliyopelekwa kwenye vyombo vya habari baada
ya chuo hicho kutajwa kama chenye wanafunzi 11 waliokamatwa Nyali juzi
kwa kashfa ya ngono, chuo hicho kilisema kina mikakati mikali ya
kufundisha maadili.
“Tunapenda kusahihisha uongo na kusema ukweli juu ya suala linaloendelea kugonga vichwa vya habari juu ya ngono
za kinyama na mbwa,” ilisema barua hiyo.
Barua
hiyo iliyotiwa sahihi na Naibu Mkuu wa chuo hicho Prof Josphat
Mwatelah ilisema, “Tungependa kuweka wazi kwa wazazi wote na umma kwamba
madai ya watu (wasichana) waliokamatwa wiki jana huko Nyali Mombasa
kwa masuala ya ukahaba na kufanya mapenzi na mbwa kuwa ni wetu ni
uongo. Wasichana hao si wanafunzi wetu wala hawahusiani kivyovyote na
chuo chetu."
Barua
hiyo iliendelea kwamba pekuapekua za stakabadhi za chuo hicho kikuu
hazikuonyesha hata jina moja kwamba ni la mwanafunzi wao.
“Kikosi
cha walinda usalama wetu pamoja na wachunguzi maafisa wa polisi
vimethibitisha kwamba watu hao kamwe si wanafunzi wetu”, ilisisitiza
barua hiyo.
Nakala
hiyo iliendelea, “Chuo chetu kina kitengo madhubuti cha kuelekeza
wanafunzi na kuwatia nia na maadili mema ya kijamii. Chuo chetu pia
kina kitengo madhubuti cha kuongoza wanafunzi juu ya maovu
yanayokithiri nchini Kenya,” ilisema.
Barua
ilieleza kwamba TUM imejitolea kuendeleza mafunzo bora kwa wanafunzi
wake ili hatimaye wawe wananchi wenye maadili, tabia na mienendomizuri
katika jamii.
“Tunavionya
vyombo vya habari kwa kutaja jina la chuo chetu kuhusiana na kashfa
hii na kwa kuharibu jina na sifa ya chuo chetu pasipo kuthibitisha
taarifa yenyewe kwanza na kutaka vituombe msamaha kupitia umma”,
iliongeza barua hiyo.
Suala
hiyo limezua mjadala mkali na kushutumiwa nchini na nchi za ng’ambo
huku mashirika ya dini na ya umma yakitaka uchunguzi kamili na wageni
wanaohusika kwenye njama hiyo wakamatwe, washtakiwe kasha warudishwe
makwao hatimaye.
Polisi
hapo Jumapili walidokeza kwamba wanamtafuta mwanamke mmoja kutoka
Karatina anayetuhumiwa kuzama kwenye lindi la biashara hiyo haramu na
ambaye ameingia gizani tangu wasichana hao 11 kukamatwa huko Nyali.
No comments:
Post a Comment