Vyombo vinavyohusika vimewakama watu sita, ikiwemo raia wanne wa Saudi
Arabia, kwa kuhusika na shambulizi la bomu lililoua watu watatu na
kujeruhi makumi katika kanisa Katoliki la Olasiti, Arusha
Rais Kikwete ameliita tukio hilo “tendo la kigaidi”...
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amethibitisha kuwa watu sita
wamekamatwa, ambapo kati yao wawili ni Watanzania, na Wanne ni Wasaudi
“Uchunguzi bado unaendelea,” alisema RC Mulongo, na kuongeza kuwa Wasaudi hao waliwasili Arusha Airport siku ya Jumamosi.
Aliongeza kuwa Watanzania wawili waliokamatwa ni Wakristo. Hakutoa maelezo zaidi
Mlipuko ulitokea nje ya kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Arusha
No comments:
Post a Comment