USIKOSE KUPITIA KAGERAKWETU MAGAZINE BLOG KUPATA MATUKIO MBALIMBALI KATISA SIASA,MICHEZO,UDAKU,UCHUMI ,UTALII NA UTAMADUNI.KWA MAWASILIANO ZAIDI 0764 179271
Monday, May 27, 2013
MAOMBI YAKO YANAHITAJIKA KWA SARAH MVUNGI, AFYA YAKE YAZIDI KUDORORA...!!
TUMUOMBEENI! staa wa Injili na filamu za Kibongo, Sara Mvungi ni mgonjwa anayesumbuliwa na vidonda vya tumbo na malaria ambavyo vimemfanya alazwe akiwa hoi
Akizungumza nasi kwa taabu wikiendi iliyopita kwenye Hospitali ya TMJ Mikocheni, jijini Dar alikokuwa amelazwa, Sarah alisema alianza kuugua siku tatu kabla ambapo alikuwa akitumia dozi ya malaria.
Alisema kuwa wakati akiwa kwenye dozi hiyo, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya kupata homa kali ambapo alikimbizwa hospitalini hapo huku maradhi ya vidonda vya tumbo ya muda mrefu nayo yakimsumbua.
Akiwa hospitalini hapo, akiwa na ‘dripu’ ikimiminika kwa kasi kuingia mwilini ambapo alikiri kuwa mwanzoni alikuwa na hali mbaya lakini walau kwa sasa anaendelea vizuri.
“Kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri, nilikuwa siwezi kutembea hadi nishikwe mkono, vidonda vya tumbo vinaniuma sana na homa nayo inanisumbua kwa siku tatu sijaweza kufanya kazini,” alisema Sarah ambaye pia ni nesi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment