Tuesday, May 7, 2013

KAZI IPO DEREVA ALIYEMGONGA TRAFFIC ENEO LA BAMAGA APANDISHWA TENA KIZIMBANI KWA KOSA LA UTAPELI".....!!

Huyu ndie mfanyabiashara aliyesababisha kifo cha Koplo Erikiza askari wa usalama barabarani jijini Dar katika msafara wa JK na leo amefikishwa mahakama ya Mwanzo Iringa kwa kujipatia mali kidanganyi.
 

MFANYABIASHARA mkazi  wa Mbeya ambae alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.328 BML aina ya Land Lover Discovery na kusababisha kifo cha askari mwenye namba  WP 2492 Coplo Elikiza Nnko wakati wa  msafara  wa Rais Jakaya  Kikwete  jijini Dar es Salaam ,amefikishwa mbele ya hakimu  wa mahakama ya Mwanzo Bomani mjini Iringa kwa tuhuma  za  kujipatia gari lenye thamani ya Tsh milioni 30 .

Mfanyabiashara  huyo Jackson Simbo Stivin(45) alifikishwa mahakamani leo asubuhi  akituhumiwa  kujipatia gari aina ya fuso lenye thamani ya Tsh milioni 30 ambalo ni mali ya mfanyabiashara  wa mkoani Iringa  Venansia Sanga.

Akisoma shtaka  hilo hakimu  wa mahakamani  hiyo ya Mwanzo Bomani  Mheshimiwa  Alois Masua alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo anadaiwa  kutenda  kosa  hilo Septemba 4 mwaka  2012 katika  eneo la Miyomboni mjini Iringa .

Mheshimiwa Masua  alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo baada ya  kutenda  kosa  hilo alitoweka na kujificha katika mikoa mbali mbali hapa nchini .
Hata  hivyo  alisema  kuwa  mlalamikaji katika  shtaka  hilo  baada ya  jitihada za kumtafuta  kushindikana ndipo alipofika mahakamani  Februari 15 mwaka  huu  kufungua kesi namba 61 /2013 kuhusiana na mtuhumiwa  huyo.

Alisema  kuwa  kutokana na  kufunguiliwa kwa kesi hiyo jeshi la  polisi kwa kushirikiana na mlalamikaji  waliendelea kumsaka mtuhumiwa  huyo bila mafanikio na baada ya kutokea ajali iliyosababisha  kifo cha askari  huyo  wa  usalama barabarani jijini Dar es Salaam katika msafara  wa Rais Kikwete ndipo mtuhumiwa huyo alipokamatwa baada ya  picha yake  kuonekana katika vyombo vya habari .
Mtuhumiwa  huyo amekana  shtaka  hilo dhidi yake na  mahakama kudai kuwa  dhamana yake  ipo  wazi na kuwa mdhamini anapaswa kusaini hati ya dhamana ya yenye  thamani ya Tsh. milioni 15 masharti ambayo yalitimizwa na wadhamini na mfanyabiashara  huyo kutolewa kwa dhamana hadi Aprili 25 kesi  hiyo itakapotajwa  tena.

Wakati  huo  huo ndugu  wa mfanyabiashara  huyo walionyesha  kuwazuia  wanahabari  kumpiga  picha  wala kuandika  habari  hiyo kwa madai  kuwa ni habari  ndogo ambayo jamii  haipaswi  kuijua na kumtaka mfanyabiashara  huyo  kujifungika  sura yake na kuondoka na msafara  wa magari mawili ya kifahari katika mahakamani hiyo.


No comments:

Post a Comment