MSANII KALAPINA A.K.A NABIKOKO KIBOKO YA MACHOKO AKIWA KWENYE STUDIO ZA RADIO CLOUDS FM KWENYE XXL AKIELEZEA SABABU ZA KUMUADABISHA SHOGA BENZINO PALE MAISHA CLUB
"Ukweli ni mambo ya fedheha, mdogo wetu Chidi Benz, nnacho weza kusema
mdogo wetu ni kwamba unga anaovuta sasa hivi unampeleka pabaya umeona
eeh, tena mimi kama kaka yake namshauri aachane na matumizi ya madawa ya
kulevya kwasababu mwisho wake utampeleka pabaya, mimi niko back stage
nna show yangu nipo kazini, tupo seious watu wa hiphop, miaka mingi
tulikuwa tuna nadi amani hatutaki matatizo na watu unaona bana, hawa ni
watu ambao kwa namna moja ama nyingine wanasababisha hiphop ishindwe
kwenda mbele na kusababisha hiphop ishindwe kwenda mbele na kuwapa
mafanikio watu wa hiphop.tumeandaa show yetu nzuri, ilikua bonge ya show
moja kali ya hiphop Tanzania kuwahi kutokea, show ambayo imekutanisha
wasanii wakali wa hiphop ambao sasa hivi wanavuma, mi niko back stage
naskia sauti ya Chidi Benz ameshika mic, muda ambao mi natakiwa kuwa
stage naperfom, sa Chidi Benz ametokea wapi mbona kwenye ratiba yetu ya
show hayupo, anaongea ubabe anakamba.yupo stage mi niko back stage bado,
mi nikawaambia watu wangu vipi, huyu mtu mbona mnamuachia anatuharibia
show? hasa watu ujue, ujue msanii, yaani jana ndio nimekubali msanii ni
mtu mwenye hadhi na heshima kubwa sana sema Chidi Benzi amejishushia
hadhi yake na heshima yake .Watu wakawa wanashindwa kumfanya kitu
wakiangalia huyu ni mtu maarufu anajulikana, watu wakawa wanamplease
kiustaarabu, Chidi eeh shuka hii show haikuhusu, sasa watu walivyokuwa
wanamplease akawa anaona labda watu mafala au nini umeona eeh.BY GWALU FUKUDA kupitia kagerakwetumagazine.blogspot.com .HARAKATI ZINAENDEeeeeeeeeeeeeeeeeee.....
No comments:
Post a Comment