Thursday, May 9, 2013

DEREVA AZIMIKA BARABARANI

Na Gladness Mallya
MWANAUME mmoja aliyetambulika kwa jina la Joseph Mwaleni anayedaiwa kuwa ni dereva wa kituo kimoja cha redio Bongo (jina tunalihifadhi), alikutwa amezimika ghafla na kuuchapa uzingizi barabarani akiwa kwenye gari lake.






Dereva Joseph Mwaleni akiwa amezima ndani ya gari alilokuwa anaendesha maeneo ya Sinza-Afrikasana.

Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza-Afrikasana ambapo Joseph akiwa kwenye foleni alipitiwa na usingizi mzito na magari yalipoanza kutembea gari lake liliendelea kusimama hali iliyosababisha foleni kuwa kubwa ndipo walipotokea wasamaria wema wakalisukuma mpaka pembeni huku njemba huyo akiwa amelala fofofo.





No comments:

Post a Comment